Wednesday, May 13, 2015

Wolper: Anayetoka na Nay wa Mitego Ameshajulikana



 Staa wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper, amewaweka njia panda mashabiki wake kwa kauli yake kwamba msichana aliyekwenye uhusiano wa kimapenzi na msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ameshafahamika, tofauti na alivyokuwa akihisiwa yeye.



“Watu hawana dogo, ukiwa karibu na mtu basi utaambiwa mpenzi wako, Nay hakuwahi kuwa mpenzi wangu kwa kuwa ni zaidi ya rafiki kwangu, ila watu wasio waelewa ndiyo walikuwa wakivumisha kwamba tuna uhusiano kwa maslahi yao, lakini sasa ukweli umejulikana kama mnavyoona na mnavyosikia Nay ni wa nani,” alieleza Jacqueline bia kumtaja anayetoka na mwana hip hop huyo.
Wolper aliongeza kwamba taarifa hizo ziliposambaa alipata tabu ambapo alikuwa akitumia muda mwingi kujieleza kwa watu wake wa karibu kutokana na tuhuma hizo.

0 comments:

Post a Comment