Lulu Atamani Kuimba Injili
Staa wa bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema anatamani sana siku moja kuimba muziki wa injili kwa vile anacho kipaji cha uimbaji.
Staa huyo aliyasema hayo wakati akihojiwa kwenye kipindi cha televisheni cha The Sporah Show wiki hii.
“Napenda kuimba...nadhani naweza kuimba, napenda kama siku ikitokea nimekuwa muimbaji niimbe gospel, napenda sana gospel" alisema Lulu.
Pia Lulu alisistiza kuwa yeye ni mtu mwenye hofu ya Mungu.
“I’m God fearing yaani namuogopa sana na namuheshimu sana Mungu sio kumuogopa peke yake. Kwahiyo pamoja na yote ninayoyafanya imani yangu ipo palepale hata mungu anajua.
Mnanijua kwa nje , huo ndio upande mnaoujua, kuna upande wangu wa ndani na hauwezi kuujua lazimu muwe watu wa ndani sio kila mmoja anaweza kuujua”-Lulu alisisitiza.
0 comments:
Post a Comment