Friday, May 1, 2015

HEKAHEKA ILIYOMKUTA BANANA ZORRO MPAKA AKAMUA KUHAMA MTAA


Kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM kulikuwa na msanii Banana Zorro akiwa na bendi yake ya B Band.. Unajua wasanii nao huwa wanaishi maisha ya kawaida kama watu wengine tu mtaani, kuna wakati wanakutana na Hekaheka pia yani !!






Kabla ya kusimulia Hekaheka yake, Banana amepiga story kuhusu ishu ya wasanii wa zamani kupotea, mwenyewe amesema wanamuziki wa sasa wana umaarufu lakini hawajafikia uwezo wa wanamuziki wa zamani.

Tukija kwenye Hekaheha aliyokutana nayo Banana amesimulia ishu aliyowahi kukutana nayo zamani wakati anaishi kwenye mtaa mmoja unaoitwa Kambauone na rafiki yake.. kilichomkuta ni kwamba huo mtaa ukileta mbwembe wanakufanyia mambo ya kiswahili.

Banana amesema aliwahi kushuhudia gari likinasa kibarazani, ikampa hofu sana akaamua kuhama mtaa.

Story nyingine ambayo Banana ameshea na sisi amesema mama yake aliwahi kumwambia kuwa asimuumize mwanamke yoyote wala kumpiga.. hajawahi kuchepuka wala kufumaniwa kwa sababu yeye kama kioo cha jamii anapenda kuwa mfano wa kuigwa.

Kusikiliza stori yote bonyeza play hapa chini…




0 comments:

Post a Comment