IMEFICHUKA! Ile ndoa ya wasanii wa filamu za Kibongo, Salome Urassa ‘Thea’ na Michael Sangu ‘Mike’ ambayo imekuwa ikiyumba mara kwa mara chanzo kimedaiwa kilianzia kwenye ufungaji wake.
[adsenseyu1]
Salome Urassa ‘Thea’ na Michael Sangu ‘Mike' siku ya ndoa yao.
Sosi wetu makini aliyeomba hifadhi ya jina lake alitutonya kuwa, ndoa ya mastaa hao ni ya mseto kwani hakuna aliyekuwa tayari kufuata imani ya mwenzake jambo lililowashangaza wengi.
“Siku ndoa inafungwa kanisani Thea hakulishwa sakramenti kwa kuwa alikuwa na imani ya kilokole na Mike alikuwa Romani Katoliki, hali hiyo ilileta kutofautiana mara kwa mara hata walipoingia kwenye ndoa,” kilidai chanzo hicho.
Akifafanua juu ya madai hayo Mike alisema: “Ni kweli tulifunga ndoa ya mseto lakini tangu tumefunga hii ndoa hatujawahi kuwa na amani.
“Kwa mwaka naweza kusema Thea anakaa kwangu miezi mitatu, hiyo mingine yote tukigombana kidogo tu anaenda kwao, ipo siku nitafanya maamuzi magumu,” alisema Mike.
0 comments:
Post a Comment