Thursday, May 7, 2015

Mastaa waahidi kujitokeza kwa wingi kwenye show ya kuchangisha fedha za matibabu ya mke wa Mabeste Jumapili hii

Lisa anasumbuliwa na maradhi mbalimbali likiwemo tatizo kwenye ubongo wake. Hivi karibuni Mabeste amekuwa akiendesha kampeni ya kuchangisha fedha kulipia gharama za matibabu yake.

Mastaa walioahidi kuwepo kwenye show hiyo ni pamoja na Vanessa Mdee, Adam Juma, Millard Ayo, Nchakalih, Roma, Diva, Young Killer, Jokate, Hemedy, Kajala, Rose Ndauka, Country Boy na Riyama.

Wengine ni Manecky, Mirror, Pam-D, Quick Rocka, Kajala, Tundaman na wengine.

Kiingilio kwenye show hiyo ni shilingi 10,000 tu.

0 comments:

Post a Comment