Diamond Platnumz na Nay wa Mitego wameamua kuyageuza maumivu yao ya kutoswa na wapenzi wao kwenye ngoma yao ‘Mapenzi au Pesa’ inayotarajiwa kutoka leo.
Wawili hao wamerekodi vipande vifupi vya video wanavyoviweka kwenye Instagram wakijibizana kuhusu mapenzi na pesa na wameamua kujilipua kweli.
“Kha! Huyu nae anakuwaga Boya sometimes… we akili yako unaona kila kitu kinataka pesa tu.. hayo mambo ndio yalokufanya kile kidem chako cha Mwanza kikuchune halaf mwisho wa siku watu wamekipa viuno ipaswavyo, kiulainiiii wamejichkulia, Unabaki kutwa kuhaha na Mtotoemoji… Mwanamke anatakiwa Ufundi, Madoio, Manjonjo kwa bed emoji UMENISKIA @naytrueboy ???,” ameandika Diamond.
Diamond amemaanisha mpenzi wa Nay wa Mitego, Siwema waliyezaa naye mtoto wa kiume aitwaye Curtis.
Nay wa Mitego naye amepost picha hiyo juu na kuandika:
“Jamani eeh?!! Embu tuongee ukweli, hivi huyu ndugu yetu @diamondplatnumz Angekua na hali iyo apo kwny picha, Je!? Ange weza kua Uyo Mwanamke apo @zarithebosslady na unadhani uyu #Zari angemkubali? Kama c vijisenti na huu umaarufu alio nao?!”
0 comments:
Post a Comment