Fareed Kubanda aka Fid Q ni mtu wa mambo tofauti. Ndio maana kuanzia mwaka huu na miaka mingine, hatotumbuiza kwa kutumia CD, bali atakuwa akichana mistari na live band.
“Nimeona nimekuwa kwenye muziki kwa muda mrefu and takriban mwaka wa 15 kila siku tunapanda stejini pale tunaperform na kwa CD na nini, najiskia tu sasa hivi acha tu niwe mwanamuziki kabisa kwakuwa nafanya kila kitu na bendi,” Fid aliiambia 255 kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM jana
“Uzuri wa kufanya show na bendi ni mmoja, si tu watu watakuwa wanaokuwa una talent peke yako, pia wanaweza kuwa wanaona mtu anapiga drums vizuri, mtu anapiga gitaa vizuri, piano. Kunakuwa na vionjo vingi mtu anakuwa anaenjoy.”
Kutokana na mabadiliko hayo, Fid amesema hata bei ya kufanya show kwa sasa imebadilika kwakuwa atakuwa akihitajika kuwalipa watu wengi pia.
0 comments:
Post a Comment