Katika miaka ya karibuni muziki Bongo umepata nafasi kubwa ya kupenya katika soko la Afrika na kimataifa kwa ujumla. Video za wasanii wa Tanzania zimekuwa zikipata nafasi ya kuoneshwa kwenye TV kubwa za kimataifa na wasanii wa Tanzania wamekuwa wakipata nominations kwenye tuzo mbalimbali za kimataifa, na miongoni mwa wasanii wa mwanzo kabisa kupata connection hizo alikuwa ni Ambwene “AY” Yessaya.
Bongo 5 imezungumza na AY kutaka kufahamu yeye kama msanii mkubwa ambaye alianza kutengeneza channel zake mwenyewe za kimataifa kwa muda mrefu, kwa nafasi aliyonayo amewasaidia vipi wasanii wenzake mpaka sasa kwa manufaa ya muziki wetu.
“kwanza kifupi ni kuwa connection(s) kubwa zote zinazoonekana kuzaa matunda sasa mimi ndio chanzo chake” alisema AY.
“Mimi ndio nili’introduce management za wasanii wa bongo kwa wasanii wa Nigeria hata hao kina Godfather wa video, part yangu ndio ilikuwa muhimu kuliko zingine zote sababu hakungekuwa na uwezekano wa chochote kutokea bila mahusiano,kufahamiana baina ya wasanii now,kwa namna gani nimesaidia wenzangu,well,ningeweza kukaa na connections zangu kivyangu,nikabana,mengi yanayotokea leo hii yasingekuwa yametokea”.
AY ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake ‘Zigo’ ameelezea kusikitishwa kwake na jinsi ambavyo wasanii aliowahi kuwasaidia kwa namna moja au nyingine wameshindwa kutambua mchango wake kwao pale wanapofanikiwa kupitia njia alizowapa.
“si lazima watu wakisaidia watu wapite mabarabarani kutangaza,ila nimesikitishwa kusikia baadhi ya wasanii wanasema sitoi connections za nje, na waliosaidiwa wanajua ukweli vile navyopambana watu wasonge mbele.”
Kupitia kampuni yake ya Unity Entertainment, AY amekuwa akiwapa deals baadhi ya wasanii ikiwa ni pamoja na deal za show za nje, kuwaunganisha na vituo vya radio na TV za nje pamoja na kuwezesha baadhi ya collabo za wasanii wa Tanzania na wasanii mbalimbali wa Afrika.
Hata hivyo hakuwa tayari kutaja majina ya wasanii aliowasaidia lakini amesisitiza kuwa ni wengi na wanajifahamu.
Friday, May 1, 2015
Home »
AY
,
Hot za Bongo
» Nimesikitishwa kusikia baadhi ya wasanii wanasema sitoi connections za
nje – AY
0 comments:
Post a Comment