Tuesday, May 12, 2015

Collabo nyingine ya Diamond na Davido? Salam, meneja wa Diamond ametupajibu

Diamond Platnumz ana collabo na P-Square, Flavour na wasanii wengine wakubwa wa Nigeria lakini pia meneja wake, Babu Tale naye aliwahi kusema kuna collabo nyingine itakuja kati ya Davido na Diamond.

Meneja wake mwingine, Salam amezungumza na Bongo5 kuelezea mradi wa mastaa hao wawili waliowahi kupishana kauli miezi kadhaa iliyopita licha ya kutengeza historia ya collabo iliyofanikiwa zaidi ya ‘Number One Remix’

“Haikukalimika bado so hatuwezi kusema kama iko tayari au bado kwasababu kuna vitu ambavyo havijamalika,” amesema Salam.

“Kuna vitu ambavyo vinatakiwa virudishwe huku, Diamond aingize vocal, amalizie ndio iweze kukamilika.”



0 comments:

Post a Comment