[adsenseyu1]
Wakazi ni msanii wa Hip Hop wa Tanzania aliyepata nafasi ya kukutana na kupiga picha na mastaa wengi wakubwa wa Marekani.
Wakazi na Wiz Khalifa
Kutokana na kuonekana akiwa amepiga picha na mastaa kama Wiz Khalifa, Kanye West, Diddy na wengine, amekuwa akiulizwa kama alifanikiwa kufanya collabo hata na mmoja wa mastaa hao.
Wakazi na Kanye West
“Ujue watu wengi wanasema ooh unapiga picha haujatoa collabo, wewe huwezi kukutana na Kanye West tu halafu ukaomba collabo wakati jamaa yuko kwenye game muda mrefu, cha muhimu ni kujifunza hivyo vitu.” Wakazi aliiambia E-Newz ya EATV.
“Nimekutana na K.R.S One, nimekutana na Rakim the best Hip Hop artist, nimekutana na kina Wiz Khalifa, Kanye West, nimekutana hata na P-Diddy nikapiga naye picha.”
Wakazi amesema alikuwa akitumia fursa ya kukutana na wasanii hao kujifunza mambo mengi kupitia wao.
“Kitu cha muhimu unapokutana na watu kama hao ni kujifunza kutoka kwao kwanza, kwahiyo inamaanisha kwamba mimi nilijielekeza kwenye kujifunza kutoka kwao zaidi […] Maana kipindi kile kumbuka hata bongo nilikuwa sijatoa hata single, siwezi kutaka kuimba na Wiz Khalifa wakati hata single hujawai kutoa hata moja na yeye hajui uwezo wako. Kwahiyo unamskiliza unajifunza kutoka kwake kwanza, unatenda halafu ukija baadae kukutana naye tena akaona ulichokitenda then itajulikana kinafanyika nini after that.” alimaliza.
0 comments:
Post a Comment