Saturday, May 2, 2015

MAJAMBAZI 15 YAVAMIA NA KUIBA NYUMBANI KWA ALI KIBA

Usiku wa jana haukuwa mzuri kwa Ali Kiba. Wakati Diamond na mpenzi wake Zari wakifurahia katika Zari All White Party iliyofana, majambazi wapatao 15 walivunja na kumvamia Ali Kiba nyumbani kwake Kunduchi, kadri ya maelezo yaliyopatikana ilikuwa kiasi cha saa tisa usiku majambazi hao waliporuka ukuta na kuvunja mlango wa sebuleni kisha kuwapiga vijana waliokuwa wamelala sebuleni. Katika kipigo hicho inasemekana majambazi hao walikuwa wanaulizia kama Ali Kiba yupo, ambapo kwa ujasiri vijana hao walisema hayupo na kuonyesha chumba cha mdogo wake Ali Kiba anaeitwa Abdu, majambazi hao waliingia humo na kuanza kuvunja na kuiba vitu kadhaa zikiwemo shilingi milioni 2 na nusu taslim. Polisi waliitwa na kufika muda si mrefu baada ya hapo. Inasemekana wakati wa tukio hilo Ali Kiba alikuweko chumba kingine na hakuonekana. Pole sana Ali Kiba. Ushauri kwa wasanii ambo wanamafanikio, si jambo zuri kujitangaza unaishi wapi na una mali kiasi gani. Utamaduni wa kutangaza katika social media kila mali uliyonayo ni hatari kwani unawatangazia hata wenye nia mbaya na ambao wanaweza kutumia taarifa yako mwenyewe kukudhuru.

[adsenseyu1]


 

0 comments:

Post a Comment