Showing posts with label Hot za Bongo. Show all posts
Showing posts with label Hot za Bongo. Show all posts

Thursday, May 14, 2015

DOWNLOAD NEW MUSIC | NEY WA MITEGO FT DIAMOND PLATNUMZ



CLICK BELOW TO GET THE SONG

Nay wa Mitego & Diamond Platnumz - Mapenzi au Pesa

BASATA Yalaani Tabia Chafu za Shilole

BASATA Yalaani Tabia Chafu na Isiyo na Maadili Iliyooneshwa na Msanii Shilole Kwenye Onesho Lake Nchini Ubeligiji


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa na burudani nchini limeona picha chafu na zisizo na maadili za Msanii Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole alipokuwa akifanya onesho lake nchini Ubeligiji hivi karibuni.

Katika picha hizo ambazo zimelaaniwa na watanzania wengi nchini kupitia njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii, Shilole anaonekana akiwa Jukwaani huku viungo vyake vya sehemu za siri vikiwa hadharani na zaidi akionesha tabia ambazo kwa kiasi kikubwa zimefedhehesha na kuidhalilisha sekta ya Sanaa na Taifa kwa ujumla.

Aidha, BASATA limepokea malalamiko kwa njia ya simu na mawasiliano ya internet kutoka kwa watanzania waishio ughaibuni wakilaani tukio la Msanii huyo. Katika mawasiliano yao wameeleza kwamba wamefedheheshwa na kudhalilika na tabia hiyo chafu iliyooneshwa na msanii huyu.

Ikumbukwe kwamba, Shilole ni msanii aliyesajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa, hivyo anapokwenda nje ya nchi kabla hajapata visa anapewa barua ya utambulisho kama msanii wa Tanzania, hivyo anapokuwa nje ya nchi anatambuliwa kama msanii Mtanzania, anapofanya kinyume na misingi ya kazi ya Sanaa, anajifedhehesha yeye mwenyewe, kazi ya Sanaa na nchi yetu pia.

Aidha, ikumbukwe kwamba BASATA limeshapata kumwita na kumuonya msanii huyu kutokana na tabia yake ya kutokujiheshimu pale awapo jukwaani na yeye aliahidi kubadilika na kuachana na tabia hiyo chafu. Kwa hiyo kuendelea kwake kufanya matukio hayo na kwa sasa katika ardhi ya nchi nyingine ni uthibitisho kwamba hajabadilika na kwa maana hiyo ameendelea kuidhalilisha Sanaa na wasanii wa kitanzania wenye kujitambua na kuiheshimu Sanaa kama kazi nyingine.

BASATA linapenda kueleza kwamba;

Litamuita kwa mara nyingine tena kumtaka ajieleze kwa nini alifanya onesho hilo la kujidhalilisha na kudhalilisha hadhi ya mwanamke, msanii na Sanaa kwa ujumla

Kama maelezo yake hayataridhisha hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake maana tayari ameshadhihirisha kwamba akifanyacho si Sanaa na hakina uhusiano na kazi ya Sanaa ambayo ina heshima yake na inahitaji ubunifu, weledi na kujitambua

BASATA linawakumbusha wasanii wote nchini kuwa Sanaa ni kazi kama kazi zingine lakini siku za hivi karibuni wasanii wengi wamekuwa wakikiuka suala zima la maadili kwa kutengeneza kazi chafu zisizofaa mbele ya jamii ya watanzania wanaoipenda na kuiheshimu kazi ya Sanaa yenye staha. Tuungane kwa pamoja kukemea kazi chafu zinazozalishwa na wasanii wasiojitambua kwani suala la maadili ni suala mtambuka na linaanzia katika ngazi ya familia.

Aidha, BASATA linawataka Wasanii wote nchini kufuata sheria, kanuni na taratibu mara wanapopata mialiko ya kikazi kwenda nje ya nchi. Linawakumbusha kwamba haiwezekani msanii kutumia picha chafu na mavazi dhalili na kuonyesha utupu katika kuvuta mashabiki.

Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini

Godfrey Mngereza

KATIBU MTENDAJI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Wednesday, May 13, 2015

Wolper: Anayetoka na Nay wa Mitego Ameshajulikana



 Staa wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper, amewaweka njia panda mashabiki wake kwa kauli yake kwamba msichana aliyekwenye uhusiano wa kimapenzi na msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ameshafahamika, tofauti na alivyokuwa akihisiwa yeye.



“Watu hawana dogo, ukiwa karibu na mtu basi utaambiwa mpenzi wako, Nay hakuwahi kuwa mpenzi wangu kwa kuwa ni zaidi ya rafiki kwangu, ila watu wasio waelewa ndiyo walikuwa wakivumisha kwamba tuna uhusiano kwa maslahi yao, lakini sasa ukweli umejulikana kama mnavyoona na mnavyosikia Nay ni wa nani,” alieleza Jacqueline bia kumtaja anayetoka na mwana hip hop huyo.
Wolper aliongeza kwamba taarifa hizo ziliposambaa alipata tabu ambapo alikuwa akitumia muda mwingi kujieleza kwa watu wake wa karibu kutokana na tuhuma hizo.

Mashabiki Wachukizwa na Picha Hizi za Aunt Ezekiel

Staa wa bongo movies, Aunt Ezekiel amepondwa na baadhi ya mashabiki wake kwa kupiga picha hizi akionyesha tumbo lake ukigingatia yeye ni mjamzito.Picha hizi zimekuwa zikisambaa kwa kwenye mitandao ya kijamii na wengi wameonyesha kuchukizwa na tabia iliyozuka ya mastaa wa Bongo kufanya hivi kwa kuwaiga mastaa wa nchi za ughaibuni.

Wewe je, unamaoni gani juu ya hizi

Shilole: Huyu Ndio Mwanaume wa Maisha Yangu

Staa wa Bongo Movies na Bongo Fleva, Shilole leo mtandaoni ameibuka na mtandaona na kuweka wazi kuwa mchumba wake Nuh Mziwanda ndio mwanaume wa maisha yake.


“Huyu nilienae pembeni yangu ndo baba yangu rafiki yangu faraja yangu ya moyo na anajua umuhimu wangu kuliko mtu yeyote yupo na mimi bega kwa bega ninapokuwa na furaha nahata ninapokuwa na majonzi mimi naweza sema ndo mwanaume wa maisha yangu naomba Mungu asije badilika nitaumia sana.Nampenda sana huyu mtu nyinyi mnamuta Nuh mimi namuita Jackson”-Shilole ameeleza.

Hili ni jambo jema,kila la kheri Shilole na Mziwanda kwenye maisha yanu ya mapenzi

OGM! .....IRENE UWOYA RELEASES SEXY PHOTOS WHILE TAKING A SHOWER IN ABATHTUB




Through instagram actress Irene Uwoya shared these hot pics of herself being in a bathtub with no piece of cloth to cover her hot chest............



Diamond na Nay wa Mitego waja na matani ya ukweli namna walivyoporwawapenzi wao sababu ya pesa (Video

Diamond Platnumz na Nay wa Mitego wameamua kuyageuza maumivu yao ya kutoswa na wapenzi wao kwenye ngoma yao ‘Mapenzi au Pesa’ inayotarajiwa kutoka leo.

Wawili hao wamerekodi vipande vifupi vya video wanavyoviweka kwenye Instagram wakijibizana kuhusu mapenzi na pesa na wameamua kujilipua kweli.

“Kha! Huyu nae anakuwaga Boya sometimes… we akili yako unaona kila kitu kinataka pesa tu.. hayo mambo ndio yalokufanya kile kidem chako cha Mwanza kikuchune halaf mwisho wa siku watu wamekipa viuno ipaswavyo, kiulainiiii wamejichkulia, Unabaki kutwa kuhaha na Mtotoemoji… Mwanamke anatakiwa Ufundi, Madoio, Manjonjo kwa bed emoji UMENISKIA @naytrueboy ???,” ameandika Diamond.

Diamond amemaanisha mpenzi wa Nay wa Mitego, Siwema waliyezaa naye mtoto wa kiume aitwaye Curtis.

11262798_836864009729992_873086903_n

Nay wa Mitego naye amepost picha hiyo juu na kuandika:

“Jamani eeh?!! Embu tuongee ukweli, hivi huyu ndugu yetu @diamondplatnumz Angekua na hali iyo apo kwny picha, Je!? Ange weza kua Uyo Mwanamke apo @zarithebosslady na unadhani uyu #Zari angemkubali? Kama c vijisenti na huu umaarufu alio nao?!”



Tuesday, May 12, 2015

Hakuna playback tena, hip hop naitumbuiza na live band – Fid


Fareed Kubanda aka Fid Q ni mtu wa mambo tofauti. Ndio maana kuanzia mwaka huu na miaka mingine, hatotumbuiza kwa kutumia CD, bali atakuwa akichana mistari na live band.







“Nimeona nimekuwa kwenye muziki kwa muda mrefu and takriban mwaka wa 15 kila siku tunapanda stejini pale tunaperform na kwa CD na nini, najiskia tu sasa hivi acha tu niwe mwanamuziki kabisa kwakuwa nafanya kila kitu na bendi,” Fid aliiambia 255 kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM jana

“Uzuri wa kufanya show na bendi ni mmoja, si tu watu watakuwa wanaokuwa una talent peke yako, pia wanaweza kuwa wanaona mtu anapiga drums vizuri, mtu anapiga gitaa vizuri, piano. Kunakuwa na vionjo vingi mtu anakuwa anaenjoy.”

Kutokana na mabadiliko hayo, Fid amesema hata bei ya kufanya show kwa sasa imebadilika kwakuwa atakuwa akihitajika kuwalipa watu wengi pia.



Kajala Anaendelea Vizuri Baada ya Kupigwa Chupa Usoni

Staa wa Bongo Movies, Kajala Masanja anaendelea vizuri baada yakupigwa chupa na kijana mmoja usiku ya kuamkia jana wakiwa kwenye show ya mwanamziki Mabeste aliyoiandaa ili kuchangisha pesa kwa ajili ajili ya matibabu ya Mkeo.

Leo kupitia ukurasa wake mtandaoni, kajala ameweka picha hiyo hapo juu  na kuandika  “Maisha yanaendelea au sio......” kuonyesha kuwa yupo poa na anaendelea na masiha yake yakawida.

Akilezea tukio hilo la kupigwa na chupa hapo jana alipofanya mahojiano na mtangazaji Millard Ayo wa Clouds FM kajala alieleza

“Mpaka tumemaliza show, sasa kwenye muda wa kuondoka nikamwambia Meneja wangu amuite msanii wetu mmoja anaitwa Tausi ili tuondoke, sasa wakati nataka kushuka kwenye gari natembea tu sijui chochote nikashangaa chupa imenipiga usoni, nikadondoka na kubiringita kwenye zile ngazi, kuna mkaka na mdada wakaniona wakanisaidia”

Akaongeza kuwa;

“Aliyenipiga na hiyo chupa ni Mwanaume, simjui na wala sijawahi kumuona hata mara moja…. amekamatwa yuko Osterbay Polisi, nilivyotoka Maisha Club nilipelekwa Hospitali Mwananyamala nimeshonwa usoni aliponiumiza, tukarudi Polisi nikaandika maelezo”.

Pole sana Kajala

Kauli ya Shilole na Mchumba Wake Juu ya Picha Chafu za Shilole Akiwa Stejini



Haya ndiyo maelezo ya wawili hao kuhusiana na picha za mwanadada shilole zikimuonyesha  wazi sehemu ya kifua chake wakati akiwa stejini anatumbuiza huko nchini Ubelgiji.

Show ni movement na uwezi mkataza mtu kupiga picha ukiwa kwa stage'na kuna nguo za show na nguo za kutoka out kikawaida'ukiruka ruka sana sidiria ni rahisi kuchomoka akina dada mnafaham na mtu yupo stejini anakua hajitambui kama nini kimetokea coz yupo stejin kwenye mood ya kazi na kila mtu ni binadamu na ndio mana wengine wanateleza kwa stage huyo paparazi aliopiga picha alifanikiwa kuzoom na kipata picha mbaya lakin katika hali ya kawaida na watu waliokua wakicheza nae hawakuweza kugundua lolote'na kiubinaadamu kama muhandishi wa habari hakupaswa kuchagua picha ambayo kaonekana vibaya mana naamini alipata picha nyingi nzuri tu za kupost ila aliamua tu kumchafua'So Mashabiki kumbukeni alikua yupo kazini hakupanga itokee ivyo na yote mradi atoe burudani nzuri kama mlivyomzoea''ambae hana upeo mdogo wa kufikiria ataongea shit ila kaa jiulize ingekutokea wewe ungesemaje? naomba mtusaidie kurepost hii habari tunawapenda sana

Nuh Mziwanda

 

Siri yafichuka Kumbe ni Ali Kiba Ndio Anaye Mnyima Usingizi Mrembo JOKATE

Lile fumbo tuliokuwa tumefumbiwa na Mwanadada Mrembo na Mjasiria Mali Jokate la mtu kumyima usingizi sababu ya Penzi lake limefumbuliwa na imebainika kuwa mtu huyu ni Mwanamuziki Ali Kiba...

Ila Wadakuz wa Ubuyu wanasema huenda watu hawa ni wapenzi wa siri wa muda mrefu kwani wamekuwa wakionekana pamoja mara kwa mara sehemu za Starehe na Jokate mara kwa mara huenda nyumbani kwa Ali Kiba bila Sababu yoyote....

Baada ya Jipu kupasuka Jokate alihojiwa lakini akashindwa kusema chochote na kuishia kujichekesha tu ,,,,

NGASSA ASAINI MIAKA 4 FREE STATE, ALAMBA $80,000,MSHAHARA $5,600, NYUMBA GARI BURE



Ni baada Yanga kumshusha thamani.Sasa awa lulu bondeni.

Gari atakayopewa ni mpya kabisa BMW made ya S.AFRICA.

Kila la kheri NGASSA.

My take:

Yanga wamuuze na Msuva,otherwise nae ataondoka free mwezi jan.

Collabo nyingine ya Diamond na Davido? Salam, meneja wa Diamond ametupajibu

Diamond Platnumz ana collabo na P-Square, Flavour na wasanii wengine wakubwa wa Nigeria lakini pia meneja wake, Babu Tale naye aliwahi kusema kuna collabo nyingine itakuja kati ya Davido na Diamond.

Meneja wake mwingine, Salam amezungumza na Bongo5 kuelezea mradi wa mastaa hao wawili waliowahi kupishana kauli miezi kadhaa iliyopita licha ya kutengeza historia ya collabo iliyofanikiwa zaidi ya ‘Number One Remix’

“Haikukalimika bado so hatuwezi kusema kama iko tayari au bado kwasababu kuna vitu ambavyo havijamalika,” amesema Salam.

“Kuna vitu ambavyo vinatakiwa virudishwe huku, Diamond aingize vocal, amalizie ndio iweze kukamilika.”



DIAMOND Flies to Dubai to Shop For His Unborn Princess

Diamond seems to be getting ready for the birth of his baby girl in style. He recently flew to Dubai to shop for his unborn baby and he proved that he has a good eye for beautiful girlish stuff.

Look at what he bought for her;

Somewhere in Dubai someone couldn’t make up thier mind. Decisions, Decisions!!!!!

 

Monday, May 11, 2015

BOW WOW AJITOA NDANI YA CASH




Taarifa zinasema kwamba rapper na mtangazaji aliyekuwa chini ya usimamizi wa Cash money, inayomilikiwa na billionea namba 5 wa hip hop duniani Birdman, Shad “Bow wow” Moss ameondoka na kuachana na lebo hiyo.Kwa mujibu wa video ya dakika 28 aliyopost kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Bow wow ameelezea kumuheshimu na kumkubali Kinoma Birdman na ametetea uondokaji wake kuwa ni wa amani.“Napenda nimshukuru sana Birdman na namuheshimu pia, alitumia muda wake kunisain pale Cash money,ninaondoka na ni kwa amani tu wala hakuna ubaya wowote alionitendea na hatujakoseana” alisema Bow Wow.Well hatua hiyo imekuja wakati ambapo kunamgogoro mwingine uliopo katika lebo hiyo, kati ya boss wa Cash money Birdman na boss wa “YMCMB” lili wyne. Imefahamika Bow wow alieanza ku rap tangu akiwa na umri wa miaka mitano 5 anakwenda kuungana kikazi na mkali Jarmine Dupri na rapper Snoop Doggy.

Picha: Wolper Awakuna Wengi kwa ‘Style’ Hii ya Aina Yake

 Wolper156 WOLPER99


Staa wa Bongo Movies  ambaye anasifika kwa urembo na kazi zake, Jacqueline Wolper hivi juzi kati kwenye ukurasa wake  mtandaoni alibandika picha hizo hapo juu akiwa amevalia style ambayo iliwafanya mashabiki wengi bonyeze kitufe cha LIKE na kushusha comment nyingi huku kila mtu akielezea ni jinsi gani ameguswa na mtindo huo aliotupia.Kwa maneno ya lugha yta malkia, Wolper aliandika “Fashion is just another accessory for someone with great style...” na kuweka picha hizo.Japo wengi walizisifia kwa kusema hiyo ni style tu na ukizingatita yupo nyumbani ame-relax, lakini pia wapo walioziponda kwa kudai hazina maadili. Yote kwa yote kama unamfuatilia staa huyu mitandaoni utakubalina nami kuwa huyu ni moja kati ya mastaa wa Bongo Movies wanaopenda fasheni, pongezui kwa hilo.

Baada ya Diamond Kuponda, Wema Sepetu ‘Amsapoti’ Kiba


Kitoka Mitandaoni: Baada ya hapo juzi Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnum kupitia ukurasa wake mtandaoni kutoa lawama juu ya uteuzi wa vipengele wa tuzo za muziki za Kilimanjaro Music Awards za mwaka huu na pia kueleza kuwa yeye hata hamasisha watu wampigia kura yapo kuwa ametajwa kuwania vipengere vingi zaidi kwenye tuzo hizo, hali nitofauti kwa upande wa pili ambapo Staa wa Bongo Movies Wema Sepetu na team yake wamekuwa mstari wa mbele kumpigia debe Ali Kiba ili watu wampigia kura ili anyakuwe tuzo zote.Kitendo cha Wema ambaye alikuwa ni mpezi wa Diamond  kumsapoti Ali Kiba ambaye kwasasa inaonekana ndiye msanii mwenye ushindani (Kisanaa) na Diamond kimechukuliwa kwa mitazamo tofauti na mashabiki wa  mastaa hawa.

Team za mastaa hawa mtandaoni maarufu kama Team Mond, Team Kiba na Team Wema wamekua na mitazomo tofauti juu ya hiki anachokifanya Wema na hadi kufikia kutoleana lugha chafu wakati team Diamond wanaponda; huku team Kiba na Wema kuwa upande mmoja.

“Unapenda kiba wakati umetemwa na chibu alafu hukumbuki arusha umefukuzwa kwa show ya kiba aibu huna kweli we mdada team platnamz hapa”-mmoja alikomenti

Team Wema na Team Kiba wanamuunga mkono

“Halafu watu wengine viazi sana humu ndani kapostiwa King king king kiba mara ooooh chibu who is the Chibu by the way haaaaaaaaa. Acheni usechu kma ni diamond huko huko kwenu uhanithi hatutaki siye halaaaaa hata kama ajibebisha mwataka ajibebishe kwenu khaaaaa. Hebu legooooooo  Wematwende sawa. Vote for King baaaaanaaaa Ama niniiiiiiiii”-mmoja alikomenti

Wema Sepetu akiwa ndiye staa wa bongo mwenye followers wengi zaidi kwenye mtandao picha wa instagram (587,000 hadi sasa) amekuwa akiweka ‘posters’ za Ali Kiba na kuandika maneno ya kumsifia kama;

“Im thinking Eye candy.... Dats da right post...”

“Too much cuteness on this poster tho......”

“Im thinking Eye candy.... Dats da right post...”

“Campaign Inaendelea ama nene.... Such a cutie...!!! Like I said, either he gets it or nat, He still Fiiiiiiiiiiiiine....! Hihihihihi.... JustSayin...!!!”

NB: Mara kadhaa Wema kwenye mahojinao amekua akisema wazi kuwa yeye ni mshabiki wa Diamond.

Mtoto abebwa sandukuni na kusafirishwa

Mtoto aliyebebwa ndani ya sanduku



Mtoto mmoja wa miaka minane amesafirishwa hadi nchini Uhispania kutoka Morroco akiwa ndani ya sanduku kwa mujibu wa maafisa wa polisi wa Uhispania.


Mvulana huyo kwa jina Abou alipatikana ndani ya sanduku hilo lililokuwa limebebwa na msichana wa miaka 19 kuelekea Cueta,eneo lililo karibu na taifa la Morrocco siku ya alhamisi.

Wakati polisi walipolifungua sanduku hilo, mvulana huyo alikuwa katika hali mbaya sana.Mvulana huyo kutoka Ivory Coast sasa anahudumiwa na mamlaka ya Cueta.

Gazeti la Uhispania El Paris liliripoti kwamba msichana huyo wa miaka 19 hana uhusiano na mtoto huyo na kwamba alilipwa na babaake ili kubeba sanduku hilo.

Babaake mtoto huyo anaishi katika visiwa vya Conary na kwamba alitarajia kuonana na mwanawe kulingana na gazeti hilo.

[adsenseyu1]
Mtoto aliyebebwa ndani ya sanduku
Chombo cha habari cha Uhispania Efe kimesema kuwa babaake mvulana huyo ambaye anajulikana kama Abou alisafiri hadi nchini Ivory Coast kumchukua mwanawe baada ya kuhamia katika eneo la Gran Canaria mwaka 2013.

Babaake baadaye aliripotiwa kumlipa raia huyo wa Morocco ambaye alimsafirisha mtoto huyo kupitia sanduku.

Msemaji wa polisi aliiambia Efe:''Alionekana kusita na kama ambaye hakutaka kupitia mpakani''.

Wimbo wa Vanessa Mdee ‘No Body But Me’ uko namba 1 kwenye Top Ten ya Radio ya Nigeria

 [adsenseyu1]





Baada ya Kichupa cha wimbo mpya wa Vanessa Mdee ‘No Body But Me’ aliomshirikisha rapper wa Afrika Kusini ‘K.O’ kuingia kwenye chati za vituo vya runinga vya kimataifa kama MTV Base na Trace, audio yake pia iko kwenye Top Ten ya kituo cha radio cha Lagos, Nigeria.

vee3

Wiki hii wimbo huo umeshika nafasi ya kwanza kwenye African Top 10 ya The Beat 99.9 Fm ya Lagos.

The beat

Nafasi ya pili kwenye chati hiyo imekamatwa na Maurice Kirya wa Uganda na wimbo wake ‘Never Been Loved Before”.

Pia kwenye chati ya Africa 10 ya Trace Urban, Video ya Vanessa na K.O imekamata nafasi ya 5 wiki hii.

trace africa ten



Friday, May 8, 2015

Wakazi aeleza kwanini haikuwa rahisi kufanya collabo na kina Wiz Khalifa, Kanye West na Diddy alipokutana nao






[adsenseyu1]

Wakazi ni msanii wa Hip Hop wa Tanzania aliyepata nafasi ya kukutana na kupiga picha na mastaa wengi wakubwa wa Marekani.
Wakazi na Wiz Khalifa

Kutokana na kuonekana akiwa amepiga picha na mastaa kama Wiz Khalifa, Kanye West, Diddy na wengine, amekuwa akiulizwa kama alifanikiwa kufanya collabo hata na mmoja wa mastaa hao.

Wakzi na Kanye
Wakazi na Kanye West

“Ujue watu wengi wanasema ooh unapiga picha haujatoa collabo, wewe huwezi kukutana na Kanye West tu halafu ukaomba collabo wakati jamaa yuko kwenye game muda mrefu, cha muhimu ni kujifunza hivyo vitu.” Wakazi aliiambia E-Newz ya EATV.

“Nimekutana na K.R.S One, nimekutana na Rakim the best Hip Hop artist, nimekutana na kina Wiz Khalifa, Kanye West, nimekutana hata na P-Diddy nikapiga naye picha.”

Wakazi amesema alikuwa akitumia fursa ya kukutana na wasanii hao kujifunza mambo mengi kupitia wao.

“Kitu cha muhimu unapokutana na watu kama hao ni kujifunza kutoka kwao kwanza, kwahiyo inamaanisha kwamba mimi nilijielekeza kwenye kujifunza kutoka kwao zaidi […] Maana kipindi kile kumbuka hata bongo nilikuwa sijatoa hata single, siwezi kutaka kuimba na Wiz Khalifa wakati hata single hujawai kutoa hata moja na yeye hajui uwezo wako. Kwahiyo unamskiliza unajifunza kutoka kwake kwanza, unatenda halafu ukija baadae kukutana naye tena akaona ulichokitenda then itajulikana kinafanyika nini after that.” alimaliza.